Polisi waanza uchunguzi tukio la Ole Sendeka kupigwa risasi

Jeshi la Polisi nchini Tanzania, kupitia kwa Msemaji wake David Misime, amebainisha kuwa wameanza uchunguzi kuhusu tukio la Mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka ambaye gari lake lilishambuliwa kwa risasi na yeye akiwemo ndani pamoja na dereva wake lakini hawakupata madhara.

Tukio hilo lilitokea jana Ijumaa Machi 29, 2024 katika kijiji cha Ngabolo wilayani Kiteto, Mkoa wa Manyara wakati Ole Sendeka akiwa safarini kutoka Dodoma kwenda jimboni kwake Simanjiro mkoani humo.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Machi 30, 2024.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *