
Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza limewafungia kuendesha Magari Kwa kipindi cha miezi sita Madereva tisa kwa makosa mbalimbali ikiwemo mwendo kasi na kutozingatia Sheria za usalama barabarani.
Hayo yamesemwa Disemba siku ya 23 2024 na Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza Naibu kamishina wa Polisi Wilbroad Mutafungwa alipokuwa akiongea na waandishi wa habari pamoja na madereva katika kituo cha mabasi Nyamhongolo mkoani Mwanza.


