Baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Mwanza wamefanya ukaguzi wa vyombo vya moto sambamba na kutoa elimu ya usalama barabarani ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Kamanda wa Polisi Mkoani hapo Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Wilbroad Mutafungwa aliyoyatoa hivi karibuni katika kuelekea mwisho wa mwaka.
Katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mwanza, Askari wa Kikosi hicho wameendelea kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto kama mabasi yaingiayo na yaendayo mikoani, magari makubwa ya mizigo, daladala, huku ikishuhudiwa madereva wakipimwa kilevi.