Kamanda wa Polisi ya Jimbo la Lagos, ametangaza kutoa zawadi nono ya kiasi cha Naira Milioni 1 sawa na Tsh/= Mil 3.2 kwa atakayefanikisha kupatikana kwa msanii Owodunni Ibrahim maarufu kama Primeboy, anayesakwa kuhusiana na kifo cha Mohbad.
Msanii huyo Prime boy alitakiwa kujisalimisha polisi kwaajili ya mahojiano maalumu ya kubaini nini chanzo cha kifo cha Mohbad kilichotokea tarehe 12 Septemba, ila hajafika.
Kabla ya tangazo hili la Polisi, Primeboy aliwahi kukanusha madai yaliyowahi kutolewa kuwa alimpiga Mohbad na anahusika na kifo chake. Washutumiwa wengine ambao mpaka sasa wanashikiliwa na polisi ni Naira Marley na Sam Larry yani wapo rumande kwa sasa.