Jeshi la Polisi Nchini, limemtaka aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole kufik katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), ili atoe maelezo na ushahidi kuhusiana na tuhuma ambazo amekuwa akizitoa kupitia mitandao ya kijamii.
Kupitia taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini, hii leo Septemba 15, 2025 imeeleza kuwa mbali na kukusanya ushahidi, pia limekuwa likifanya jitihada za kumpata Polepole ili aweze kutoa maelezo na vielelezo vitakavyothibitisha tuhuma hizo, kwa ajili ya kuchukua hatua za kisheria.
