kurugenzi Mtendaji Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Mohamed Janabi, ameonya wanaofanya mazoezi ya kukimbia maarufu kama ‘jogging,’ kuwa wako kwenye hatari ya kuanguka na kupoteza maisha ghafla.
Amesema mauti inaweza kuwakuta watu wa aina hiyo kama ambavyo inatokea kwenye viwanja vya mpira wa miguu, iwapo watakuwa hawajatambua afya zao hasa wale wenye ugonjwa wa moyo.
Profesa Janabi amesema hayo wakati akielezea utekelezaji wa majukumu na mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu hiyo kwa mwaka wa fedha 2023/24.