Kipa namba moja wa Klabu ya Yanga SC, Djigui Diarra huenda akawa nje ya Uwanja kwa Wiki sita akiuguza majeraha yake ya kigimbi na nyama za paja ambayo yamekua yakimsumbua.
Daktari wa timu hiyo Moses Etutu amelishauri benchi la ufundi kutomtumia Golikipa huyo ili apatiwe matibabu apone kabisa sababu kumtumia mchezaji huyo akiwa na majeraha wanaweza kumkosa kwa muda mrefu zaidi.
Kwa tafsiri hiyo, Diarra huenda akakosa michezo yote ndani ya kipindi hicho ikiwemo ya Ligi kuu na mitatu ya Ligi ya mabingwa Afrika (CAF Champion League) dhidi ya TP Mazembe January 03 (Home) dhidi ya Al Hilal January 10 (Away) na dhidi ya MC Alger January 17 (Home).