Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewasili katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Hosea Kutako, ukioko Windhoek chini Namibia.
Rais Samia amefika Nambia kwa ajili ya kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa Rais wa Namibia Marehemu Dkt.Hage Geingob, tarehe 23 Februari, 2024.
Shughuli za Mazishi za Rais huyo Hayati Dkt. Hage Geingob zinatarajiwa kufanyika katika Jiji la Windhoek tarehe 24-25 Februari, 2024.