Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameandaa dua ya kumuombea hayati Mzee Mwinyi ambaye amefariki dunia tarehe 29 Februari 2024 katika hospitali ya Mzena, Dar es Salaam na kuzikwa tarehe: 02 Machi 2024 Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Waumini wa dini ya Kiislamu, Ndugu na waombolezaji wameshiriki katika Dua hiyo ya khitma ambayo imefanyika leo tarehe 03 Machi 2024, katika viwanja vya maonesho Nyamanzi, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.







