PICHA: Odinga, Ruto na Museven wakutana na kufanya mazungumzo

Moja kati ya picha zilizoibua hisia nyingi za Watu wengi ni uwepo wa picha za Wanasiasa na Viongozi kutoka Kenya na Uganda, picha inayomuonyesha Rais wa Uganda Yoweri Museven, Rais wa Kenya William Ruto na Kiongozi wa upinzani Kenya Raila Odinga.

Kupitia Mtandao wa X, Odinga alipost picha hizo na kusema ‘Siku kadhaa zilizopita, nilikubali mwaliko wa Rais Yoweri Museveni wa Uganda, kuwa na mkutano wa pamoja na Rais William Ruto, kujadili kuimarika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Muhimu zaidi kwa kuhimizwa na Rais Museveni, tulijadili pia kugombea kwangu Uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika’ – Odinga.

‘Ninamshukuru sana Rais Museveni kwa kuidhinisha kwa dhati kuteuliwa kwangu na kwa Rais Ruto kwa kuunga mkono kikamilifu, Baada ya hapo tulipata muda nje ya shughuli zetu nyingi kutembelea shamba la ng’ombe la Rais Museveni huko Kisozi’ – Odinga.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *