Mkuu wa Wilaya ya Misungwi ambaye alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Johari Samizi leo tarehe 12 March, 2024 amemkabidhi Ofisi Mkuu wa wilaya mpya wa Shinyanga Julius Mtatiro mara baada ya uhamisho uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 9 March, 2024 ambapo awali Mtatiro alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru.

Akizungumza katika makabidhiano haya samizi amemshuru sana Rais kwa kuendelea kumuamini na kwenda kuwatumikia wananchi wa Misungwi huku akiishukuru kamati ya ulinzi na usalama pamoja na wakurugenzi kwa ushirikiano mzuri alioupata katika kutimiza majukumu mbalimbali na kumueleza Mhe. Mtatiro kuwa anamuachia Wilaya ya Shinyanga ikiwa na amani na utulivyo hivyo asiwe na wasiwasi.
“Kipekee namshuru sana Rais wetu Dkt. Samia kwa kuendelea kuniamini na kunipeleka kwenda kuwatumika wananchi wa Misungwi, niwashuru pia kamati ya ulinzi na usalama pamoja na wakurugenzi kwa ushirikiano mzuri mlionipa Mhe. Mtatiro nakuachia wilaya ya Shinyanga ikiwa na amani na utulivu na usihofu utapata ushirikiano mkubwa zaidi katika majukumu mbalimbali.”amesema Samizi

Kwa upande wake Mtatiro amemshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu kwa kuendelea kumuamini na kumleta kuja kuwahudumia wananchi wa Wilaya ya shinyanga na kuwaomba kamati ya ulinzi na usalama pamoja na wakurugenzi kumpa ushirikiano katika majukumu mbalimbali ili waweze kuwahudumia vizuri wananchi wa Shinyanga.
“Imempendeza Rais kwa kibali cha Mwenyezi Mungu kunituma kuja kuendeleza gurudumu la maendeleo hapa shinyanga lakini pia niwashukuru kwa mapokezi mazuri mlionionesha nimefurahi namna mnavyoendelea kufanya mjukumu yenu ya kila siku kikubwa naomba ushirikiano mzuri ili tuweze kuwahudumia wananchi wetu wa shinyanga.”amesema Mtatiro.
