Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeendelea na maandamano ya amani kwenye mkoa wa Arusha, Baada ya Dar, Mbeya na Mwanza.
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe ameongoza maandamano hayo Mkoani Arusha ambayo yanategemewa kuhitimishwa kwenye uwanja wa Relini uliopo Arusha Mjini sehemu utakapofanyika mkutano wa hadhara wa Chama hiko.