Categories

Do you have a Story?

Call us on 0677 644 444 to submit your news story or incident report!

Paul Pogba kufungiwa miaka minne

Kwa mara nyingine tena Paul Pogba amekutwa na hatia ya matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni baada ya matokeo ya vipimo vya awamu ya pili kubaini kuwa alitumia dawa za kusisimua misuli.

Awali Mnamo Septemba 11, 2023 Pogba alisimamishwa kwa muda na Mahakama ya Kitaifa ya Kupambana na Utumiaji wa dawa za kusisimua misuli ambapo aliomba ufanyike uchunguzi wa sampuli ya pili kwa ajili ya kuhakiki matokeo ya kipimo cha kwanza.

Chini ya Kanuni ya Kuzuia Matumizi ya Madawa ya Kulevya, Mfaransa huyo atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha miaka minne, ambacho kinaweza kupunguzwa kwa nusu iwapo atathibitisha kwamba hakutumia dawa hizo kwa makusudi.

Mbali na taratibu za mfumo wa haki za michezo wa Italia, uchunguzi wa kimahakama utafunguliwa na ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma wa Turin, kwani dawa za kuongeza nguvu ni kosa la jinai nchini Italia

Pogba ana siku saba za kuwasilisha utetezi wake kwenye Mahakama ya Kitaifa ya Kupambana na Dawa za Kulevya, ambayo itachunguza kesi yake kabla ya kutekeleza adhabu hiyo utaratibu ambao unaweza kuchukua wiki kadhaa.

Kufuatia sakata hilo klabu ya Juventus imemsimamisha mshindi huyo wa kombe la Dunia 2018 kufanya mazoezi ya klabu hiyo huku ikisitisha malipo ya wastani wa mshahara wake wa Euro milioni 8 kwa mwaka hadi 2026.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *