Staa wa Afrobeat kutoka Nigeria, Patoranking, amekula shavu kwa kupata ubalozi wa kampuni ya Choice International Group (CIG), watengenezaji wa bidhaa za Lontor (vifaa vya umeme majumbani).
Patoranking alitambulishwa kama balozi siku ya jana, Jumatatu huko Lagos na katika hotuba yake aliwataka vijana wa Nigeria, kujilinda na kuepuka matumizi mabaya ya dawa za kulevya, kwani wanahatarisha fursa zao katika kuleta na kuchangia maendeleo ya taifa