PAPA RASMI AONEKANA HADHARANI, ATOA NENO

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis (88), ametokeza hadharani kwa mara ya kwanza baada ya kulazwa Hospitali ya Gemelli iliyopo jijini Roma Italy, kwa zaidi ya Mwezi mmoja sasa.

Papa ambaye leo hii ametoa Baraka za jumapili kwa waumini, pia aliwaaga wafanyakazi wa Hospitali hiyo na kurejea Vatican, baada ya Madaktari kumshauri kujizuia kukutana na makundi makubwa ya watu au kufanya shughuli za kumchosha.

Hadi sasa bado haijajulikana iwapo ataweza kuongoza ratiba za matukio muhimu ya kidini hasa kuelekea siku kuu ya Pasaka kufuatia ushauri huo wa Madaktari.

One response to “PAPA RASMI AONEKANA HADHARANI, ATOA NENO”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *