Panya mmoja amekamatwa kwa madai ya kumwaga chupa 60 za pombe haramu zilizohifadhiwa katika kituo cha polisi huko Madhya Pradesh, India.
Polisi wakikabiliwa na hali ya sintofahamu wakijiandaa kuwasilisha pombe hiyo iliyokamatwa mahakamani, wanahusisha unywaji huo wa ajabu na panya wanaokaa kwenye jengo hilo kuukuu.
Licha ya mashaka hayo, wanadai kuwa wamemkamata panya mmoja ‘mtuhumiwa’ na kupanga kumfikisha mahakamani kama ushahidi.