
Timu ya Soka ya Pamba Jiji FC, kutoka Jijini Mwanza imepata mdhamini wa jezi kutoka Netsports ya Dar es salaam ambapo wameingia makubaliano ya utengenezaji na uuzaji wa jenzi za timu hiyo kwa muda wa miaka miwili.
Darisi Bujaga Mkurugenzi wa Kampuni ya Netsports amesema wameamua kuwekeza kwenye timu ya Pamba Jiji Fc kutokana historia ya klabu hiyo sambamba na ukubwa wake ambao umesababisha kuwa na mashabiki wa Asili.
Kwa upande wake Frank Mvati Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza ameipongeza Netsports kwa udhamini wa jezi za wachezaji na mashabiki ikiwa ni moja ya nguzo mkubwa katika kusaidia timu kufikia malengo yake.