Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini Moshi mkoani Kilimanjaro imemuachia huru aliyekuwa Kasisi wa Parokia ya Mt. Dionisi ,Aropagita Kawawa wilayani Moshi baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha pasipo shaka tuhuma ya ubakaji na ulawiti wa mtoto wa miaka 12 zilizokuwa zikimkabili.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Jennifer Edward amekariri vifungu kadhaa vya sheria na kusema ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka umekuwa dhaifu kukidhi matakwa ya kisheria.
Padri huyo alifikishwa mahakamani mwaka 2022 na kufunguliwa kesi tatu tofauti ikiwemo hii namba 44 ya mwaka 2022.


