Staa wa muziki kutoka Nigeria, Omah Lay, ambaye mwaka Desemba 12,2020 alilala mahabusu nchini Uganda baada ya kukiuka kanuni za COVID-19 ila tukio hilo lilimkuta pamoja na Tems na Meneja wake Muyiwa amebainisha kuwa tukio hilo ni baraka kwakwe.
Omah Lay anafunguka katika mahojiano aliyofanya na Beat FM ya London kuwa yeye na Tems walizuiliwa na kufunguliwa mashtaka, na kuhukumiwa kifungo nchini Uganda baada ya kukiuka kanuni za umbali wa kijamii wa COVID-19 kwa kushiriki tamasha katika Hoteli ya Speke -Kampala.
Ila siku iliyofuata, waliachiliwa kutoka mahabausu, na mahabusu ambayo kwenye seloalikuwa yeye NA Meneja wa Tems, Muyiwa [Awoniyi], awalik alikuwa akilitazama tukio hilo kama mkosi ila kwa sasa analitamazama kama baraka.