Ofisi ya Mkurugenzi wa mashtaka ikamilike kabla ya Jan 2, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mndeme amemtaka mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa ofisi ya Mkurugenzi wa mashitaka uliopo katika mtaa wa Miti Mirefu kata ya Mjini Halmashauri Ya Manispaa ya Shinyanga kuongeza nguvu na muda wa kazi ili kukamilisha ujenzi huo na kuhakikisha ifikapo January 2 mwaka 2024 jengo hilo linaanza kutumika kutokana na makubaliano ya mkataba wa ujenzi huo.

Mndeme ametoa maelekezo hayo wakati akikagua ujenzi wa ofisi hiyo mpya ya mkurugenzi wa mashitaka mkoa wa Shinyanga ili kujionea maendeleo ya mradi huo huku akisema jengo hilo ni la kwanza kwa ukubwa katika ukanda wa ziwa Victoria na wananchi watapata huduma za msaada wa kisheria na kudai haki zao katika jengo hilo.

Awali akitoa taarifa juu ya maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo mkandarasi anayesimamia mradi huo kutoka kampuni Elerai Construction Mhandisi Hussein Msuya amesema ujenzi huo umefikia asilimia 60 huku akianisha kuwa jengo hilo lilianza kujengwa mwaka 2022 na ameahidi kukamilisha mradi huo kwa wakati.

Ofisi ya Mkurugenzi wa mashitaka mkoa wa Shinyanga haikuwa na jengo la kufanyia kazi zake kwa kujitegemea hali iyopelkea serikali ya wamu ya sita kutoa jumla ya shilingi bilioni 2.1 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa mradi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *