Baadhi ya raia wa Nchini Kenya, wamekuwa na maoni tofauti baada ya Kinara wa Upinzani na Waziri Mkuu wa zamani wa Taifa hilo, Raila Odinga baada ya kushindwa katika uchaguzi wa Uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AUC).
Raia hao,kwa nyakati wamemtaka Odinga kushirikiana na Raisi William Ruto kuendesha Taifa, huku wengine wakisema kwasasa aweke nguvu katika upinzani, ili kuipa Serikali changamoto za kiutendaji kitendo kinachotafsiriwa kama ni chabkusuka ama kunyoa.

Odinga licha ya kupigiwa upatu wa ushindi, lakini alishindwa katika kinyang’anyiro cha mgombea Mwenyekiti wa AUC, nafasi ambayo imechukuliwa Waziri wa Mambo ya nje wa Djibouti, Mahamoud Ali Youssouf.
Mahamoud alishinda Odinga ambaye alikuwa mwakilishi pekee kutoka Afrika Maahariki, aliyeongoza duru mbili za kwanza na kupoteza katika mzunguko wa tatu.