NZWALILE AWAITA WANANCHI KUSIKILIZA SERA ZA DKT. SAMIA MANYARA

Na Afarah Suleiman, Babati – Manyara.

Katibu wa Siasa na Uenezi wa chama Cha mapinduzi (ccm) mkoa wa Manyara, John Nzwalile, amesema kuwa mgombea wa Urais kupitia chama hicho, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwasilia katika mkoa huo Oktoba 3. 2025 kuendeleza kampeni za CCM kwa kunadi ilani ya chama na kuomba ridhaa ya wananchi kuendelea kuongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nzwalile amesema kuwa mara baada ya kuingia Manyara akitokea Arusha, Dkt. Samia atafanya kampeni zake kwenye majimbo mawili ambapo ataanza mikutano kwa wananchi wa mji wa Magugu wilayani Babati na baadaye kuelekea wilayani Hanang’.

Aidha, ameongeza kuwa Oktoba 4 /2025, mgombea huyo wa urais atakuwa wilayani Babati, katika viwanja cha stendi ya Zamani,ambapo anatarajiwa kuzungunza na wananchi katika viwanja hivyo na kuomba ridhaa ya kumchangua katika uchaguzi mkuu unatarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.

Katika hatua nyingine Nzwalile amewataka wananchi wa Manyara kujitokeza kwa wingi kumpokea na kumsikiliza mgombea huyo wa Urais kuoitia chama cha mapinduzi CCM, akisisitiza kuwa chama kimejipanga kuhakikisha kila mmoja anapata nafasi ya kushiriki katika kampeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *