Mchezaji wa timu ya soka ya Real Madrid na Timu ya Taifa ya Ufaransa Aurelien Tchouameni ameweka ngoma ya Single Again, kutoka kwa #harmonize kama miongoni mwa ngoma anazozikubali.

Ngoma hiyo inapatikana kwenye albamu mpya ya Harmonize iitwayo Visit Bongo.

Aurelien Tchouameni ameweka taarifa hiyo katika Insta Story yake ambapo aliorodhesha idadi ya ngoma zaidi ya kumi ambazo anazikubali za Afro Beat na Rap, na katika orodha hiyo kuna wasanii kama Rema, Davido, Asake, Wizkid, Eminem, Drake, Kendrick Lamar na wengineo.
