Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia Kamati Tendaji ya Kanda ya Serengeti yenye Mikoa ya Mara, Simiyu na Shinyanga kwenye kikao chake cha Jumatano Januari 8.2025 kilichoketi Shinyanga, Kimeamua kumvua Uongozi aliyekua Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Shinyanga Emmanuel Ntobi.
Kamati hiyo imefikia maamuzi hayo kutokana na Ntobi kukiuka maadili na utovu wa nidhamu ikiwemo kuchafua Viongozi wa Chama chake Kitaifa kupitia mitandao yake ya Kijamii.
Katibu wa CHADEMA Kanda ya Serengeti, Jackson Mnyawami, amenukunuliwa akisema
“Tunapenda kuujulisha Umma kuwa, kuanzia sasa Emmanuel Ntobi siyo Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Shinyanga” – Mnyawami