Meneja wa Huduma za kibenki Kutoka Benki Kuu ya Tanzania BOT, Mtwara, Melchiades Domino Rutayebesibwa amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha mavuno kwa kujikita zaidi kulipana fedha kupitia mitandao ya simu au Benki badala ya pesa mikononi ili kuepuka kulipwa noti bandia.

Akizungumza Mjini Songea wakati akitoa elimu kuhusiana na utambuzi wa noti bandia, amesema kwa mwaka 2025 bado hawajapoke taarifa yoyote ya uwepo wa noti bandia lakini ni muhimu wananchi kuendelea kuchukua tahadhari na kutumia njia ya miamala ya simu kukamilisha taratibu za mauzo ya mazao yao.