Na Cecilia Shiratu, Bukoba – Kagera.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, Jacob Simon Nkwera ameeleza kuwa wanatambua changamoto iliyopo katika utekelezaji wa mradi wa TACTIC, katika ujenzi wa Kingo za mto kanoni uliochelewa kuanza na hivyo kupelekea changamoto kwa wananchi wanao ishi katika kata hizo ikiwemo kata ya Bakoba, Bilele, Nshambya, Hamugembe, kagondo na Rwamishenye.
Nkwera ameyasema hayo katika Kikao cha robo ya nane ya mwaka 2025/2026 na kusema kiwepo kikao cha pamoja kati ya madiwani, mshauri elekezi na mkandarasi Ili kuweka mpango kazi kwa pamoja Ili kushinikiza kuhakikisha changamoto hiyo inatatuliwa kwa haraka Ili wananchi waishi katika mazingira salama.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba, Acton Lwankomezi amesema wana wasiwasi endapo msimu wa mvua utakapofika hivyo inaweza kupelekea tena kuleta athari ya moja kwa moja kwa wananchi kutoka na kusuasua kwa ujenzi wa mradi wa ujenzi wa mto kanoni hivyo kupelekea mafuriko, vifo vya watu na kushuka kwa uchumi.
Naye Diwani ya kata ya Bilele Tawfiq Salum amemlalamikia mkandarasi kutokana na kusuasua kwa ujenzi wa mradi huo na kumuomba aangalie kipaumbele zaidi Cha wananchi katika jimbo la Bukoba mjini hivyo amewaomba madiwani kuungana kuweka Adhimio Ili kujua changamoto inayokwamisha ujenzi wa mradi wa Kingo za mto kanoni ambao unapelekea wananchi kuondoka kwenye makazi yao na kutafuta maeneo ambayo ni salama zaidi.
Nao baadhi ya wananchi katika jimbo la Bukoba mjini wameeleza kero wanayoipata kwa kuepo kwa changamoto ya Kingo za mto kanoni ikiwemo mafuriko ambayo yanapelekea vifo, kuhama kwa wananchi na kukwamisha shughuli za kiuchumi.


