Njombe ni balaa kwa VVU

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Mpango amewaasa wananchi wa Mkoa wa Njombe kuchukua tahadhari ya maambukizi ya Virusi vya UKIMWI baada ya takwimu kuonesha kuongezeka kwa maambukizi ya ugonjwa huo.

Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kufunga maonesho ya SIDO kitaifa mkoani Njombe ambapo amesema ni vyema wananchi kuchukua tahadhari kabla ya kuambukizwa.

Aidha, Dkt. Mpango amesema kuwa wananchi wa Njombe wana wajibu wa kutunza vyanzo vya maji na utunzaji wa mazingira ili kuvutia wawekezaji kutoka nje ya mkoa huo na nje ya Tanzania kuwekeza hasa sekta ya kilimo.

Akizungumza kuhusu uhaba wa maji, amewaagiza Waziri wa Maji na Waziri wa Fedha kutafuta pesa ili kutatua changamoto ya maji hasa katika maeneo yanye tatizo kubwa la upatikanji wa maji Mkoani Njombe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *