NJIA YA MIKOA YA KUSINI SASA INAPITIKA – WAZIRI ULEGA

WAZIRI WA UJENZI, Mhe. Abdallah Ulega amewataka madereva na wamiliki wa mabasi yaendayo mikoa ya Kusini kuyaruhusu kuanza safari sababu njia kwa sasa inapitika baada ya kurekebishwa kutokana uharibifu uliotokana na mvua kubwa iliyonyesha April 6 mwaka huu na kupelekea kukata mawasiliano kati ya mji wa somanga na matandu katika wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi.

Waziri Ulega ameyasema hayo baada ya kufungua njia hiyo kupitika vizuri kwa magari aina zote na kutaka wale waliokwama katika kituo cha mabasi Mbagala na wale waliokwama Mtwara na Lindi mjini kuendelea na safari kama zamani huku jitihada za kuendelea na ujenzi wa madaraja ya muda mrefu ukiendelea kutekelezwa na wakandarasi ambao bado wako saiti kwenye ujenzi wa madaraja matano yanayoendelea kujengwa katika njia hiyo.

Barabara ya kwenda mikoa ya kusini ilifungwa baada ya mawasiliano kukatika kwenye daraja la Somanga Mtama na Daraja la Matandu hali iliyopelekea abiria hao kukwama kwa siku mbili mpaka wataalamu kutoka wizara ya Ujenzi walipofanikisha kurudisha mawasiliano hayo na magari ya mizigo na abiria yakiruhusiwa kuendelea na safari.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *