” Niliwatangazia naondoka klabuni hapo na sijaandika barua”

Kocha Ernest Middendorp ambaye amedumu klabuni hapo kwa wiki mbili amesema Jumatatu (Septemba 18, 2023) katika kikao kilichoongozwa na Waziri wa Fedha ambaye ndiye Bosi wa Klabu, kulikuwa na mambo mengi ya kuingilia majukumu yake na aliona yanavuka mipaka, akaamua kuwatangazia hapo hapo kuwa anaondoka klabuni na hajaandika barua.

Amesema hayo wakati akihojiwa na Mtangazaji Robert Marawa wa Afrika Kusini, akieleza kuwa kulikuwa na hoja ya kuingiliwa kuhusu kikosi alichokipanga, pia akakanusha madai ya kupigiwa simu wakati wa mapumziko kutoka kwa Viongozi ili afanye mabadiliko ya wachezaji

Upande wa Afisa Habari wa Singida, Hussein Masanza amesema wameona taarifa hizo, lakini wanachojua ni kuwa Middendorp bado ni kocha wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *