Nilifulia na kuyumba kiuchumi mie – Iyanya

Mwaka 2020, Iyanya alikuwa amefulia na kujikuta amepoteza kila kitu ikiwemo nyumba aliyokuwa akiishi na kuishia kuishi hotelini na bili za hoteli zilimshinda, Hii ilikuwa wakati alipofikishwa kizimbani na uongozi wake wa zamani wa Temple Management, kwa madai ya “kuiba” gari la kampuni hiyo.

“Nilikuwa mahakamani kwa muda mrefu, sikufanya shoo yoyote kwa muda mrefu. Unajua, unapoacha kufanya shoo, lazima urudi kwenye akiba yako, uliyonayo na unajikuta nayo unaimaliza, kiukweli hali ilikuwa mbaya sana kwangu!! siku mbili baada ya kesi yangu ya mwisho, COVID-19 nayo ikaanza,” amesema Iyanya kupitia Poscats yaTea With Tay ya Taymesan,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *