Na Saada Almasi, Meatu – Simiyu.
Ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya kuzisaka kura kata kwa kata kijiji kwa kijiji za mgombea wa nafasi ya ubunge jimbo la Meatu, Salum Khamis Salum Jambo amepita katika kata ya Imalaseko ambako ndiko aliko zaliwa na kuzungumza na wananchi wa eneo hilo huku akiwasisitiza vijana kufumbua macho na kuziona fursa zilizopo mbele yao kwani hata yeye hakuzaliwa na utajiri bali alianzia biashara ya chimvi ambayo baba yake mzee Khamis hakumpa mtaji.
Akiwa mbele ya halaiki, Salum Jambo amesema kuwa wakati wa mabadiliko ni sasa na hakuna mtu atakaye walazimisha maendeleo isipokuwa wananchi wenyewe kuamua kupokea na kufanyia kazi fursa wanazozipata kwa kujituma.
“Mimi nimezaliwa hapa wazee mnajua,nimelala chini,nimesoma shule haina hata dawati nilipomaliza nimeanza kuuza chumvi nyie mashahidi,sikuwa na mtaji kutoka kwa baba yangu ila nilifanya (batertrade) biashara ya mabadilishano bidhaa kwa bidhaa nawapa watu chimvi wao wananipa mahindi,na sikuwaza jambo lingine lolote zaidi ya pesa leo hii ninaitikisa nchi,” amesema Salum Jambo

“Baada ya uchaguzi nitaleta makampuni manne hapa Mwanhuzi yatakopesha pembejeo za kilimo kama matrekta ya kulimia, bodaboda, guta hivyo kila kijana hapa atakuwa na kitu cha kumpa ajira na hiyo ajira si lazima uwe bodaboda, chukua pikipiki fanya biashara zitambue fursa zilizo mbele yako,”
“Ukijua katika eneo lako nini kinakosekana pita humo, mfano tu hapa hakuna samaki kabisa chukua pikipiki kalete samaki kijiji jirani uza na mimi nitafanikisha mpate hiyo mikopo kwa masharti nafuu” ameongeza Salum Jambo
Aidha kuhusiana na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi Jambo amesema kuwa sasa Meatu inakwenda kufunguka isivyo kawaida kutokana na zaini ya kilometa 160 za barabara kujengwa katika jimbo hilo ambazo zitafungua fursa za maendeleo jimbo zima hivyo ni wakati wa kujipambanua na kukubali mabadiliko

“Hapa kwenu nilianza kujenga kiwanda lakini mlinikatisha tamaa kutoa nguvu kazi ili niwalipe mlikataa mwishowe nimeacha gofu, nyumba yangu nimejenga hakuna mtu anataka kuishi hapo maana familia yangu haipo hiyo nyumba ni yenu imebidi niache kuijenga, sasa ilani ya chama changu inaelekeza ujenzi wa barabara “
“niwaambie Meatu inakuja kufunguka hadi mtashangaa, ile miaka mitano ambayo sikuwepo sasa itafidiwa na miaka mitano mtakayonipa kwa maendeleo ambayo hamjawahi kuyaona jimbo hili ila kwanza mjitambue na kukubali mabadiliko,” amesema Salum Jambo.
Kuhusiana na changamoto ya maji katika eneo hilo Jambo amewaahidi wananchi hao kudhughulikia haraka ili waendeleo kupata huduma hizo sambamba na kumalizia ujenzi wa zahanati pamoja na matundu ya vyoo katika shule ya msingi Imalaseko.

“Wakati wa uongozi wangu nilileta maji hapa mkayatumia japo ham hamkuyatumia kuwaletea maendeleo maana mnarudi nyuma kila siku,sasa kuna zahanati haijaisha na hayo matundu ya vyoo niwaambie nitamalizia ili muendelee kupata huduma muhimu mfuatilie kuna magofu mangapi ya zamani nije kumaliza,hatutaki miradi isimame hapa labda muanzishe mipya,” Salum Jambo
Hadi sasa mgombea huyo amezungumza na wananchi wa kata ya Kabondo, Ng’hoboko, Kimali, Mwamishali, Mwamanongu na Mwangudo huku maeneo mengine yakitazamiwa kufikiwa, ili kila mpiga kura wake aweze kusikia sababu zitakazo mshawishi kumpa kura hapo Oktoba 29, 2025.


