‘Niajiriwe kunyongwa’

Washiriki wa Mkutano wa haki jinai Kibaha, mkoani Pwani, wamejikuta wanabaki hoi baada ya mmoja wa wakazi mkoani humo, Ramadhani Maulidi, kueleza kuwa anatamani siku moja angeajiriwa na Serikali ili akafanye kazi ya kunyonga watu waliohukumiwa kutumikia adhabu hiyo.

Amesema kuwa amefikia hatua hiyo kutokana na taarifa zinazoelezwa na vyombo mbalimbali kuwa ni zaidi ya miaka 10 sasa adhabu hiyo imekuwa haitekelezwi, huku matukio ya mauaji yakiendelea kushamiri nchini hivyo ni vema Serikali ifikie hatua ya kuliangalia hilo ikiwemo hata kuajri watu wenye roho ngumu kama yeye ili waifanye kazi hiyo.

“Haiwezekani mtu anaua kwa makusudi halafu anaenda kukaa gerezani miaka na miaka bila kunyongwa hilo haliwezekani, kama mtu amekutwa na hatia ya kuua naye anyongwe lakini siyo unasikia wengine wanaanza kusema haki za binadamu kwani yeye alipokuwa anaua alikuwa hajui kuwa kuna haki za binadamu?”

Mjumbe wa tume hiyo, Profesa Edward Hosea, amesema kuwa katika ufuatiliajj wao wamebaini kuwa sheria nyingi zinatakiwa kufanyiwa marekebisho ili kulinda haki za wananchi.

“Hata utitiri wa majeshi unapaswa kuangaliwa na kuundiwa sheria upya kwani uwepo wake umekuwa ukileta hofu kwa jamii mfano kuna Jeshi la Zimamoto na Uokoaj na kazi yao kubwa ni kuzima moto, hawa wanapaswa kuwa taasisi tu na siyo kuwa kwenye mfumo wa jeshi,” amesema.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *