Rais wa Marekani Donald Trump amesema ni vigumu kushirikiana na Ukraine kuliko Urusi katika majaribio ya kuleta amani kati ya Mataifa hayo mawili.
Trump ameyasema hayo mbele ya Waandishi wa habari katika Ikulu ya Marekani wakati akizungumzia hali ya mapatano baina ya Mataifa hayo mawili.

Awali, Trump alisema anazingatia kwa kina kuweka vikwazo vikubwa na ushuru kwa Urusi, hadi usitishaji vita na Ukraine uafikiwe.