Na Ibrahim Rojala
Hii leo Mei 22,2024 Kampuni ya huduma za Mawasiliano nchini Tigo Tanzania imeendelea kuonesha namna inavyothamini wateja wake zaidi ya milioni 20 kwa kwenda nao Sako kwa Bako!
SAKO KWA BAKO ni msemo wa Kiswahili unaomaanisha tupo bega bega, pamoja kila hatua na kwenye hii #Tigo inasheherekea kua #sakokwabako na wateja wake zaidi ya milioni 20.
Licha ya uwepo wa sababu nyingi zilizowafanya wateja wa Mtandao huu kuendelea kuuamini,kuna sababu kuu nne za kipekee ambazo wanaendelea kujivunia kupitia Tigo Tanzania ambazo ni mtandao wa 5G wenye kasi zaidi ya 1GBPS.
Sababu ya pili ni Mtandao wa 4G uliobereshwa na unaopatikana kila kona ya Tanzania ambapo katika kila kila sehemu yenye mnara wa Tigo kuna teknologia ya 4G
Tatu ni uwepo wa vifurushi vya Saizi ya mteja vinavyompa thamani ya pesa zake na nne ni uwepo wa
#Tigopesasuperapp mpya iliyoboreshwa inayorahisisha miamala kidigitali.
🤩Tigo wanasema kwao ni Mwendo wa Sako kwa Bako tu, unyo kwa unyo, pamoja na wateja wao zaidi ya milioni 20 na wanakwambia
endelea kufurahia mtandao wa watu💙