NI OMBI LANGU LA NNE, SERIKALI IKAKUTANE NA WANAODAI FIDIA BONDE LA MTO RWICHE – CHIPANDO

Kutokana na baadhi ya Wananchi wanaomiliki maeneo yanayohusika na utekelezaji wa mradi wa Bonde la Mto Rwiche Mkoani Kigoma kutolipwa fidia, Mbunge wa Kigoma Mjini, Clayton Chipando (Baba Levo), ameiomba Serikali kwenda Mkoani humo kukutana na kufanya nao maongezi.

Chipando ametoa kauli hiyo hii leo Agosti 26, 2026 Bungeni jijini Dodoma na kuongeza kuwa utekelezaji wa mradi huo umeendelea kukumbana na changamoto kutokana na kuchukuliwa kwa maeneo ya Wananchi bila ya kuwalipa fidia.

Amesema, “naomba Mheshimiwa Waziri, hili ni ombi langu la nne katika Bunge hili, tafadhali naomba twende Kigoma ili tukakutane na Wakazi wanaomiliki maeneo ya Mto Rwiche, ukaongee nao wasikie kauli ya Serikali,” amesema Mbunge huyo.

Akijibu ombi hilo, Naibu Waziri wa Kilimo, David Silinde amesema Serikali iko tayari kwenda eneo la mradi, ili kutafuta suluhisho la kudumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *