NI MUHIMU KUPATA SULUHISHO LA KUDUMU KULETA AMANI YA DRC – RAIS SAMIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema ni muhimu kupata suluhisho la kudumu linaloheshimu uhuru wa mataifa, kukuza ushirikishwaji, na kuhakikisha kuwa watu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wanafurahia amani na usalama wa kudumu.

Rais Samia ameyasema hayo hii leo Februari 8, 2025 katuka Mkutano wa pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali wa EAC na SADC unaofanyika Ikulu, jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa ni muhimu raia wa DRC wakafurahia amani na usalama wa kudumu.

“Ni muhimu kupata suluhisho la kudumu linaloheshimu uhuru wa mataifa, kukuza ushirikishwaji, na kuhakikisha kuwa watu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) wanafurahia amani na usalama wa kudumu ambao wameutamani kwa miongo kadhaa,” alisema Rais Samia.

Rais Samia pia amesema Tanzania inaendelea kujitolea kusaidia juhudi zinazoendelea za kidiplomasia kumaliza mgogoro mashariki mwa DRC na kwamba anatoa wito kwa pande zote zinazohusika katika mgogoro wa DRC kushiriki kwa njia chanya katika mazungumzo, ili kulinda ustawi wa watu wake na maisha yenye amani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *