Ni Boston Celtics na Dallas Mavericks fainali ya NBA

Dallas Mavericks itakutana na Boston Celtics katika fainali kuu ya NBA msimu huu, baada ya kuwachapa Minnesota Timberwolves kwa michezo 4-1 kwenye fainali ya kanda ya magharibi.

Mkali Luca Doncic na Kyrie Irving kila mmoja amepiga pointi 36 na kuiongoza Mavericks kushinda vikapu 124-103 katika mchezo wa tano mjini Minnesota, alfajiri ya leo.

Hii ni mara ya kwanza Mavericks inatinga fainali kuu ya NBA tangu washinde taji lao pekee mwaka 2011, lakini ni mara ya tatu tu kwa ujumla.

Kwa upande wa mabingwa wa kihistoria Celtics wenyewe wanafukuzia taji la 18 la NBA katika fainali zao 23 walizocheza. ‘best-of-seven’ ya fainali kuu ya NBA itaaanza mjini Boston, Juni 7.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *