Rais wa Poland Andrzej Duda amezungumza kwa njia ya simu na Rais wa Congo Felix Tshisekedi ili kufanikisha kuachiliwa huru kwa msafiri na raia wa Poland aliyehukumiwa kifungo cha maisha jela katika nchi hiyo kubwa ya Afrika ya Kati, kwa mashtaka ya ujasusi, msaidizi wake amesema Jumatatu.
Raia huyo wa Poland Mariusz Majewski mwenye miaka 52, alikamatwa na vikosi vya Kongo DR mwezi Februari na baadaye alifikishwa katika mahakama ya kijeshi katika taifa hilo, akihutumiwa kwa ujasusi.
Tuhuma dhidi yake zinasema kuwa aliufikia mstari wa mbele kwa wanamgambo wa Mobondo,alisonga mbele bila idhini na kupiga picha katika maeneo nyeti na ya kimkakati, na kwa siri alichunguza shughuli za kijeshi.
Mobondo ni kundi la wanamgambo ambalo limekuwa likihusika katika ghasia za kikabila kusini magharibi mwa Kongo DRC tangu mwaka 2022.