Ngoma tatu za marehemu Mohbad zimeingia kwenye chati kubwa za muziki za Billboard, ngoma hizo zimeingia kwenye eneo la Billboard Hot Trending Songs Powered by X chart na ni mara ya kwanza kuingia kwenye chati hiyo.
Ngoma ya ‘Peace’ imeshika nafasi ya pili, ‘Feel Good’ yenyewe imeshika nafasi ya 5 na ‘Ask About Me’ imeshika namba 8.
Mohbad alifariki wiki iliyopita Jumanne na akazikwa jumatano, pia heshima za mwisho zinatarajiwa kufanyika leo katika Uwanja wa Muri Okunola- Lagos- Nigeria.