Juzi Novemba 16, lebo ya WCB ilimtambulisha msanii wake D Voice kujiunga na lebo hiyo na pia wakaachia albamu yake iitwayo Swahili Kid, yenye ngoma zipatazo 10.

Katika ngoma hizo 10, ngoma tatu pekee kutoka kwa msanii huyo ndio zimefikisha views/watazamaji zaidi ya laki moja.
Ngoma ya kwanza inayoongoza kuwa na watazamaji ni:- Kama Wengi ft Diamond Platnumz ina (161k), Mpeni ft Mbosso (127K) na Bam Bam ft Zuchu(116K).
