
NA EUNICE KANUMBA, SHINYANGA
LEO ikiwa ni siku ya tatu tangu kufunguliwa kwa zoezi la uchukuaji fomu kwa watia nia, Aliyekuwa mkurugenzi msaidizi idara ya sheria katika Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) Eustard Ngatale leo ametia nia ya kugombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini kwa kuchukua fomu katika ofisi za chama cha mapinduzi (CCM) wilaya ya Shinyanga mjini.
Ngatale amekabidhiwa fomu hiyo leo majira ya saa tatu asubuhi na katibu wa CCM wa wilaya ya Shinyanga mjini Ndugu Hamisa Chacha.