
Mfanyabiashara mmoja ambaye ni mgonjwa kutokea Brazil ameamua kumwachia mali yake yote atakapoaga dunia, hii ni kwa sababu anampenda sana mchezaji huyo.
“Nampenda na nina uhusiano na baba yake ambao unanikumbusha mengi yangu na baba yangu ambaye amefariki” alisema katika mahojiano na chombo cha habari cha Metropoles.
Neymar ambaye ni mmoja wa wanamichezo wanaolipwa vizuri zaidi duniani, akiwa na wastani wa mapato ya dola za Marekani milioni 85 kwa mwaka 2023, kulingana na Forbes.
“Sina afya nzuri na kwa sababu hiyo, nikaona sina mtu wa kumuachia vitu vyangu na nisingependa serikali au ndugu ambao sielewani nao wachukue” aliongea mfanyabiashara huyo.