Skip to main content

ZUNGU ACHAGULIWA KUONGOZA MKUTANO WA 153 IPU

Baraza la uongozi la Umoja wa Mabunge Duniani, limemchagua Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu, kuwa Rais wa Mkutano wa 153 wa umoja huo.

ZUNGU ACHAGULIWA KUONGOZA MKUTANO WA 153 IPU
Studio Narration JAMBO FM

ZUNGU ACHAGULIWA KUONGOZA MKUTANO WA 153 IPU

0:00 --:--

Baraza la uongozi la Umoja wa Mabunge Duniani, limemchagua Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu, kuwa Rais wa Mkutano wa 153 wa umoja huo.

Hoja ya kumchagua Spika Zungu kuwa Rais wa Mkutano huo imetolewa na Spika wa Bunge la Uingereza (House of Commons), Sir Lindsay Hoyle, na kuungwa mkono na baadhi ya nchi ikiwamo Uganda na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Uamuzi huo umefikiwa leo Oktoba 6, 2026, ikiwa ni siku ya pili ya Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), unaoendelea jijini Arusha katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC). #IPU153Tanzania

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.