Skip to main content

ZUIO LA MIKUTANO: CCM WAAHIRISHA SHEREHE ZA WIKI YA WAZAZI KITAIFA

Na Gideon Gregory - Dodoma.

ZUIO LA MIKUTANO: CCM WAAHIRISHA SHEREHE ZA WIKI YA WAZAZI KITAIFA

Na Gideon Gregory - Dodoma.

Kufuatia agizo la Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi kumwelekeza Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) kusitisha utoaji wa vibali vya mikutano ya hadhara kwa vyama vyote vya siasa kwa kipindi hiki, Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi CCM, Maganya Abdul Rajabu, ametangaza kuahirishwa kwa sherehe za Wiki ya Wazazi Kitaifa 2026 ambazo zilikuwa zifanyike mkoani Mwanza kuanzia Juni 30 hadi Julai 4, 2026.

‎Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma leo Juni 27,2026 Maganya amesema uamuzi huo unafuatia tamko hilo la Serikali.

‎"Maadhimisho haya yalikuwa yafanyike chini ya kaulimbiu isemayo, "Malezi Bora na Uzalendo ni Msingi wa Taifa," huku yakitarajiwa kuwakutanisha wanachama na wadau mbalimbali kutoka maeneo tofauti ya nchi katika kilele cha maadhimisho hayo," amesema. 

‎Amesisitiza kuwa kutokana na mazingira yaliyopo na maelekezo yaliyotolewa na Serikali, Jumuiya ya Wazazi imeamua kuahirisha sherehe hizo kwa muda usiojulikana hadi itakapotoa taarifa nyingine kuhusu tarehe mpya ya maadhimisho.

"Maandalizi ya maadhimisho hayo yalikuwa tayari yamekamilika katika ngazi za matawi, wilaya na mikoa, ambapo hatua iliyokuwa imebaki ni kukamilisha shughuli hizo katika ngazi ya kitaifa kwa kilele kilichokuwa kimepangwa kufanyika Julai 4, 2026,"amesema. 

‎Aidha, amewataka wanachama wa Jumuiya ya Wazazi CCM pamoja na wananchi kwa ujumla kupokea uamuzi huo kwa utulivu na kuendelea kufuatilia taarifa rasmi zitakazotolewa na uongozi wa jumuiya kuhusu hatua zitakazofuata.

‎Maganya ameomba radhi kwa wanachama, wadau na wananchi wote kutokana na usumbufu uliojitokeza kufuatia kuahirishwa kwa maadhimisho hayo, akiahidi kuwa taarifa mpya itatolewa mara baada ya mazingira kuruhusu shughuli hizo kufanyika.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.