Na Clavery Christian Bukoba – Kagera.
Serikali kupitia Wizara ya mifugo na uvuvi kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya kilimo (TADB) imeendelea kutekeleza zoezi la utoaji wa mikopo isiyo na riba na yenye masharti nafuu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya ufugaji wa samaki kwenye vizimba.
Akizungumza katika halfa ya uzinduzi wa kukabidhi mitaji ya kuwezesha utekelezaji wa miradi iliyobuniwa na Vijana wa (Build Better Tomorrow (BBT)-Uvuvi Mkoa wa Kagera-Bilolo Kemondo, Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Bi Emelda Adam amesema programu hiyo inalenga kupambana na changamoto ya ajira kwa vijana.

Naye Msimamizi Mkuu wa programu ya “BBT” kanda ya ziwa, Peter Masumbuko alisema vijana 47 wa mkoa wa Kagera wamenufaika na programu hiyo ambapo kiasi cha shilingi za kitanzania bilioni 7 zimetengwa kwa ajili ya vijana wa mikoa ya kanda ya ziwa.
Awali Mkuu wa wilaya ya Bukoba, Erasto Sima kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Kagera alimshukuru Rais wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya programu hiyo na kuwaasa vijana wanufaika wa mkopo huo kuutumia kwa malengo yaliyokusudiwa.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bukoba Naye aliishukuru serikali kupitia wizara ya mifugo na uvuvi kwa kuukumbuka mkoa wa Kagera na kuwaasa vijana kuwa na nidhamu katika matumizi ya fedha walizozipata.
Programu ya “BBT” chini ya wizara ya mifugo na uvuvi imewawezesha mitaji kwa njia ya mikopo nafuu wa vijana 308 nchini kote.


Discussion
Reader comments
0 contributions