Skip to main content

ZINGATIENI ELIMU AFYA YA UZAZI KUJIKINGA NA MIMBA ZA UTOTONI - NGAZIME

Wasichana waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano kwa mwaka wa masomo 2026/2027 wamehimizwa kuzingatia elimu ya afya ya uzazi wanayopewa na wataalamu wa afya, ili kujikinga dhidi ya mimba za utotoni ambazo zinaweza kuvuruga ndoto zao za kielimu.

Rai hiyo imetolewa na Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Tabora, Josephat Ngazime, alipokuwa akizungumza katika kongamano lililowakutanisha wanafunzi wanaofadhiliwa na Shirika la CAMFED, lililofanyika katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Tabora.

Akitoa taarifa kuhusu kongamano hilo, Mratibu wa Miradi wa CAMFED katika wilaya za Nzega na Tabora, Levina Pius, amesema jumla ya wanafunzi 231 kutoka mikoa ya Tabora na Singida walishiriki, wakipata mafunzo mbalimbali yanayolenga kuwawezesha kufikia malengo yao ya elimu na maisha.

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Bombamzinga, Elizabeth Msabila amesema, ufadhili unaotolewa na CAMFED umechangia kuwajengea wasichana uwezo wa kujiamini, kuongeza ari ya masomo na kuwasaidia kutimiza ndoto zao.

Baadhi ya wanafunzi wanaonufaika na mpango huo wameeleza kuwa kupitia CAMFED wamepata msaada wa ada, sare za shule, pamoja na mafunzo ya uongozi na stadi za maisha ambazo zimekuwa chachu ya maendeleo yao.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.