Skip to main content

ZIMAMOTO WATOA BIMA ZA AFYA KWA WATOTO 26 WENYE UHITAJI MAALUM SINGIDA

Na Saulo Stephen - Singida.

ZIMAMOTO WATOA BIMA ZA AFYA KWA WATOTO 26 WENYE UHITAJI MAALUM SINGIDA
Studio Narration JAMBO FM

ZIMAMOTO WATOA BIMA ZA AFYA KWA WATOTO 26 WENYE UHITAJI MAAL...

0:00 --:--

Na Saulo Stephen - Singida.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida limetoa bima ya afya kwa watoto 26 wenye uhitaji maalum, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha ustawi wa jamii pamoja na huduma za kimatibu kwa watoto hao.

Akizungumza wakati wa kukabidhi bima hizo,Mkuu wa Wilaya ya Singida Godwin Gondwe amelipongeza Jeshi la Zimamoto kwa hatua hiyo, akisema linaonyesha kwa vitendo dhamira ya Serikali ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya bima ya afya kwa wote.

Amesisitiza kuwa ushiriki wa taasisi za umma katika kusaidia makundi maalum ni muhimu katika kufikia maendeleo jumuishi na ustawi wa jamii.

Kwa upande wake, Mkuu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Singida, Mrakibu Devotha Bigawa amesema kuwa utoaji wa bima hiyo ni sehemu ya juhudi za jeshi hilo kuwa karibu na jamii, hasa kwa makundi yenye mahitaji maalum.

Ameongeza kuwa Jeshi la Zimamoto litaendelea kushirikiana na wananchi katika shughuli mbalimbali za kijamii na kutoa msaada pale inapohitajika.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.