Skip to main content

ZIMAMOTO KAHAMA WAFANYA ZOEZI LA UTAYARI KUYAKABILI MAJANGA

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

ZIMAMOTO KAHAMA WAFANYA ZOEZI LA UTAYARI KUYAKABILI MAJANGA
Studio Narration JAMBO FM

ZIMAMOTO KAHAMA WAFANYA ZOEZI LA UTAYARI KUYAKABILI MAJANGA

0:00 --:--

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Shinyanga kupitia Kituo cha Wilaya ya Kahama, leo limeendelea kuimarisha uwezo wa askari wake katika kukabiliana na majanga ya moto na maokozi kwa lengo la kuongeza ufanisi, weledi na utayari wa kiutendaji.

Katika mazoezi hayo yaliyoongozwa na Mkuu wa Kituo hicho mkaguzi msaidizi Hafidhi Omari, askari walifanya mazoezi ya nadharia na vitendo ya kukabiliana na majanga ya moto na maokozi.

Omari ametumia fursa hiyo kuwasisitiza Askari umuhimu wa kufanya mazoezi mara kwa mara, ili kuongeza uwezo, umakini na utayari wa kukabiliana na majanga ya moto na uokoaji kwa ustadi na ufanisi wa hali ya juu.

“Tunatakiwa kuwa tayari kila wakati kwakuwa majanga haya au ajali hazipigi hodi kwahiyo ni jukumu letu kufanya mazoezi kila wakati ili tuwe tayari kukabiliana na majanga haya” Amesema Omari.

Katika zoezi la kwanza askari wameonyesha umahiri wa kukabiliana na majanga ya moto baada ya kupokea taarifa kupitia namba ya dharura ya jeshi hilo ambayo ni 114.

Zoezi la pili askari wameonyesha umahiri wa kufanya maokozi kwenye ajali baada ya kupokea taarifa kupitia kituo cha taarifa cha jeshi hilo kwenye namba 114.

Hata hivyo Omari amesema kuwa kituo cha zimamoto na uokoaji wilayani Kahama,kina vifaa vyote vya maokozi ikiwemo gari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) na gari ya kuzimia moto.

“Wananchi wa Kahama watumie namba 114 kutoa taarifa za ajali na majanga ya moto,kito cha Kahama kwa sasa kina vifaa vya kutosha ikiwemo gari la kubebea wagonjwa na gari kubwa la kuzimia moto na askari wakutosha” Ameongeza Omari.

Nao baadhi ya wananchi wa manispaa ya Kahama wamelipongeza jeshi la zima moto na uokoaji kwa juhudi wanazofanya katika uokozi hasa majanga ya moto katika mitaa mbalimbali ya wilaya ya Kahama.

"Kwakweli mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni,zima moto Kahama wanafanya kazi nzuri sana ya uokozi hasa kwenye majanga ya moto,tunawashukuru sana lakini pia wanapokuja kwenye majanga ya moto wanatoa elimu kwa wananchi kuhusu namna ya kujikinga na majanga haya” Amesema Agnes Kessy na Ashiraf Hamza wakazi wa mtaa wa manispaa ya Kahama.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.