Skip to main content

ZAIDI YA WANANCHI LAKI NNE KUPATIWA VYANDARUA BURE VYENYE DAWA

Na Daniel Gahu - Katavi.

ZAIDI YA WANANCHI LAKI NNE KUPATIWA VYANDARUA BURE VYENYE DAWA

Na Daniel Gahu - Katavi.

Katika Kuhakikisha kampeni ya ziro Malaria inafanikiwa, wananchi zaidi ya 489,225 wa Wilaya ya Tanganyika wanatarajiwa kunufaika na kampeni ya ugawaji wa vyandarua vyenye dawa inayolenga kupunguza maambukizi ya malaria na kuboresha afya za jamii. Kampeni hiyo itatekelezwa katika kata 16 na vijiji 55, huku kaya 90,597 zikitarajiwa kufikiwa.

Maandalizi ya kampeni hiyo yamejadiliwa katika kikao kazi kilichoongozwa na Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau wa kudhibiti na kutokomeza malaria, kilichowakutanisha viongozi mbalimbali wa wilaya kwa lengo la kuimarisha mikakati ya utekelezaji.

Katika kampeni hiyo, jumla ya vyandarua 312,561 vinatarajiwa kugawiwa kwa wananchi wa maeneo yote yaliyopangwa kufikiwa ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali za kupunguza maambukizi ya malaria.

Viongozi na waratibu wa zoezi hilo katika halmashauri ya wilaya ya Tanganyika wamekubaliana kuimarisha usalama wa vyandarua wakati wa usafirishaji na ugawaji, kusimamia kwa karibu zoezi la uandikishaji wa kaya na kuhakikisha taarifa za utekelezaji zinawasilishwa kwa wakati. Wananchi wamehimizwa kujitokeza kuandikishwa ili waweze kunufaika na huduma hiyo.

Aidha, mikakati ya uhamasishaji wa jamii imewekwa kupitia vyombo vya habari, matangazo ya umma pamoja na ushirikishwaji wa viongozi wa dini na jamii ili kuongeza uelewa kuhusu matumizi sahihi ya vyandarua vyenye dawa.

Sambamba na kampeni hiyo, Serikali itaendelea kutekeleza mbinu nyingine za kudhibiti malaria ikiwemo kunyunyizia dawa katika mazalia ya mbu, kutoa elimu ya kinga na kuhamasisha wananchi kupima afya mapema wanapopata dalili za ugonjwa huo.

Baadhi ya wananchi wamefurahishwa na hatua hiyo ya kuona Serikali ikiwajali, ambapo wameitaka Serikali kupitia kwa waratibu wa zoezi hilo kutenda haki kwa kugawa vyandarua kwa kuzingatia usawa. Ambapo matamanio ya wengi ni kuona wananchi wote wakinufaika na vyandarua hivyo hususan waishio maeneo ya vijijini.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.