Skip to main content

ZAIDI YA WAKAZI 3,000 KUNUFAIKA NA AJIRA KUPITIA MAKAMPUNI YA 101 KAHAMA

Zaidi ya wakazi 3000 wanatarajia kunufaika na ajira za mojo kwa moja kupitia makampuni ya 101 yaliyopo Manispaa ya Kahama huku kipaumbele wakipewa wakazi wa Kahama na maeeno Jirani ya manispaa hiyo hali itakayosaidia tatizo la upungufu wa ajira kwa vijaa.

ZAIDI YA WAKAZI 3,000 KUNUFAIKA NA AJIRA KUPITIA MAKAMPUNI YA 101 KAHAMA
Studio Narration JAMBO FM

ZAIDI YA WAKAZI 3,000 KUNUFAIKA NA AJIRA KUPITIA MAKAMPUNI Y...

0:00 --:--

Zaidi ya wakazi 3000 wanatarajia kunufaika na ajira za mojo kwa moja kupitia makampuni ya 101 yaliyopo Manispaa ya Kahama huku kipaumbele wakipewa wakazi wa Kahama na maeeno Jirani ya manispaa hiyo hali itakayosaidia tatizo la upungufu wa ajira kwa vijaa.

Kauli hiyo, imetolewa na meneja biashara wa makapunini ya 101, Ayubu Sossy wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema katika makapuni ya 101 asilimia 95 ya watendakazi kazi ni wazawa wa Kahama huku asilimia 5 ni wataalamu mbalimbali kutoka nje ya nchi na mikoa mbalimbali ya Tanzania.

“Tunajivunia sana kuwa na watenda kazi ambao wanatuzunguka,makampuni ya 101 asilimia 95 ya wfanyakazi ni wananchi wa Kahama na asilimia chache sana ni wageni na wengine ni kutoka nje ya mkoa wa Shinyanga na kwasasa tunawafanyakazi wapatao 650na bado idadi hii itaongezeka tena katika makampuni yetu.” Amesema Sossy.

Sambamba na hayo Ayubu amesema kuwa 101 inatarajia kufungua kampuni mpya mbili ndani ya manispaa ya Kahama ambapo kampuni ya kwanza ni kampuni ya kusindika mazao na kampuni ya pili ni kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti na kwamba viwanda vyote viwili vitahitaji wafanyakazi.

“Watu wengi wanaifahamu Magic 101 ila 101 ina taasisi nyingi sana na hivi punde tunaenda kutambulisha kampuni ya kusindika mazao Pamoja na kiwanda cha kuzalisha mfuta ya alizeti kwahiyo tunatarajia kuwa na watendakazi wengi ambao si chini ya wafanyakazi zaidi ya 1000” Ameongeza Sossy.

Kwa upande wake Mkurugenzi mwenza wa makampuni ya 101 Rogers Rweyongeza amesema kuwa tarehe 24 ya mwezi huu itakuwa ni maadhimisho ya miaka mitano tang kuanzishwa kwa Taaasisi ya Magic 101 ambapo watafanya matendo ya huruma ikiwemo kuwatembelea watoto yatima na kutoa misaada ya kiutu kwa wagongwa na kwamba maadhimisho hayo ni ishara ya shukrani kwa taasisi zote za umma wanazoshirikiana nazo.

“Ndugu waandishi wa habari Nitumie nafasi hii kuwajulisha kuwa tarehe 24 mwezi huu tunaadhimisha miaka mitano ya taasisi yetu ya Magic 101,katika maadhimisho haya kama ilivyo desturi yetu tutashiriki matendo ya hisani kwa kutembelea watoto yatima lakini pia tutatoa misaada kwa wagonjwa katika hopsitali yetu ya Wilaya ya Kahama na hii ni ishara ya shukrani kwa washirika na taasisi zote ambazo tunashirikiana nazo” Amesema Rweyongeza.

Naye msemaji wa Taasisi ya Magic 101 na mjumbe wa kamati ya UbunifuZawadi Mtipa (Zedo) amesema kuwa katika maadhimisho ya miaka 5 wamejipanga kutoa burudani ya kuridhisha kwa kuleta wasanii wakubwa akiwepo Marioo na kwamba kamati ya ubunifu imejipanga kuandaa kitu cha tofauti.

“Sisi kama kamati ya ubunifu tumejipanga vizuri kuhakikisha wakazi wa Kahama na wengine watakaokuja Magic 101 wanapata burudani ya kutosha na yenye kiwango kwani tunawaletea wasanii wakubwa wenye vigezo akiwepo Marioo na wengine wengi na tuwahaidi kupata kitu cha tofauti ambacho hawajawahi kukishuhudia Kahama” Amesema Zedo.

 

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.